Jocktan Makeke: Mbunifu wa Tanzania anayetumia ngozi, mifupa, miti, makopo na vingine kutengeneza nguo
Kabla wakoloni hawajaja Afrika na kututawala, mababu zetu walikuwa wakiishi kwa kutegemea mazingira yanayowazunguka.
Mavazi waliyovaa, yalitokana na miti na vitu vingine vya asili. Baada ya mkoloni kuja na kudai kuleta ustaarabu Afrika, mengi yalibadilika. Tukipeleka mbele hadi mwaka 2017, asilimia zaidi ya 90 ya nguo ambazo Watanzania tunavaa, ni zile zilizotengenezwa nje na nyingi huja kama mitumba.
Mbunifu wa mavazi/Msanii wa mitindo, Jocktan Makeke ana jicho la tofauti katika namna anavyobuni mavazi yake. Yeye hutumia ngozi, mifupa, miti, makopo na vingine kutengeneza nguo. Katika muendelezo wa ubunifu wake wa Kiafrika, Makeke anatambulisha mkusanyiko wake wa mwaka 2017 alioupa jina, OTOSIM.
“Mara nyingi nimekuwa nikafanya mitindo ya Kiafrika inayoelezea utamaduni wa mtu mweusi kabla ya kuja wakoloni,” ameiambia Bongo5.
“Mitindo hiyo iliitwa TABID, yaani The African beauty in the Darkness. Lakin sasa kwenye hii OTOSIM naelezea haswa mitindo ya Kiafrika lakini hii natumia taka mbalimbali au mabaki yanayotokana na wanyama na mimea, kama mifupa, ngozi na taka nyingine ambazo tunaziona kwenye mazingira yetu kila siku, kama makopo ya maji, vizibo, vifuu, mifuko ya plastic na vyuma (recycling),” anaeleza.
“Nimeamua kuziita OTOSIM kwa lengo la kuonyesha kuwa sio tu nafanya mitindo inayohusu utamaduni but pia naweza kufanya mitindo inayohusiana na mazingira, – yaani kutumia takataka mbalimbali kiubunifu na kutengeneza magazine.”
“Mitindo hii ina ubunifu wa hali ya juu, kitu ambacho sio kila mtu anaweza kufikiria kufanya hivyo, na pia utengenezwaji wa nguo hizi umezingatia sana principle & elements of design.”
Makeke anasema sanaa yake ina lengo la kuwafumbua macho waafrika ambao wamejikuta wakitukuza zaidi mitindo ya kizungu na kusahau asili yao.
“Toka mwanzo lengo lilikuwa ni kukumbusha tu jamii ya sasa mambo mbalimbali yanayowahusu kama wa Afrika, na ukizingatia kuwa utamaduni wa magharibi umetukamata kwa sasa,” anasema.
“Pia kuhamasisha watu kuwa wanaweza kutumia taka mbalimbali ili kutengeneza bidhaa nyingine na kuacha mazingira yakiwa safi kabisa.
Vipi kuhusu mapokezi ya kazi zake?
“Kwa sasa zinapokelewa vizuri sana ukilinganisha na kipindi cha nyuma wakati naanza. Fashion kwa sasa Tanzania imekua kwa kiasi kikubwa sababu mahitaji ya mavazi toka kwa wabunifu yameongezeka sana, na pia show za fashion zimekuwa nyingi na huhudhuriwa na watu wengi.”
Hivi karibuni Makeke alishinda tuzo ya ia Juzi nimepata award ya DAY TO DAY AFRICAN DESIGNER kwenye Mpingo Fashion Awards.