Michezo
John Terry ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu

Klabu ya Chelsea imetangaza rasmi kuwa Nahodha wao John Terry ataondoka klabuni hapo baada ya msimu huu kumalizika.
Beki huyo ambaye ni raia wa uengereza ana umri wa miaka 36, ameichezea Chelsea mechi 713 na kufunga magoli 66 tangu ajiunge nao mwaka 1998.
Ni mchezaji wa tatu kwa kushiriki mechi nyingi za klabu hapo na amekuwa nahodha wa klabu hiyo kwa rekodi ya mara 578.