BurudaniVideos

Jose Chameleone afafanua kuhusu interview iliyotafsiriwa kuwa amemponda Diamond (Video)

Mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya, Willy M Tuva amemhoji staa wa Uganda, Jose Chameleone kuhusu kauli tata aliyoisema kwenye mahojiano na kituo cha runinga cha NTV cha nchini kwao iliyotafsiriwa kuwa amemponda Diamond.

Diamond

Alisema kuwa kwa muda mrefu watu wamekuwa wakijaribu kutengeneza kile alichokiita ‘lines za bifu’ kati yake na Diamond.

“Diamond ni msanii, mimi ni msanii pia, ana mafanikio yake na mimi nina yangu, napenda muziki wake,” alisema staa huyo. “Unajua tulikuwa kwenye TV show moja Kampala nikaulizwa maswali fulani halafu media wenyewe wakajaribu kubadilisha hiyo maneno iwe maneno ya kumtukana Diamond. Inatia aibu sana kwasababu katika tour yangu Marekani niliongea na Diamond, niliongea na Babutale na vitu kama hivyo, namheshimu kama msanii na yeye pia ananiheshimu, hivyo hakuna sababu ya kuwa na bifu, sina sababu yoyote ya kusema mambo mabaya kuhusu yeye, sikusema kitu kama hicho,” alisisitiza Chameleone.

Kuhusu uwezekano wa wawili hao kufanya wimbo wa pamoja, Chameleone alisema tatizo ni kuwa wote wako busy lakini wakipata nafasi hicho ni kitu rahisi kutokea.

Tazama mahojiano hayo hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents