Burudani

Jose Chameleone asema na ‘haters’ ‘Don’t blame me for your failure’

Nguli wa muziki nchini Uganda Jose Chameleone anasifika kwa kuwa na beef zisizokauka na wasanii wenzie ama mapromoter wa muziki. Bila shaka unakumbuka beef yake na Erick Shigongo. Jana kupitia ukurasa wake wa Facebook ameandika dongo ambalo halijulikani linamwendea nani lakini ni wazi linaenda kwa miongoni mwa wapinzani wake.

Chameleone anamwambia mtu huyo asiyejulikana kuwa suala la kumlaumu yeye kwa kufeli kwake ni sawa na kupakaza ujinga.

“Blaming me for your failure is alleging nonsense against me. I have been on top of the charts for a decade and somehow managed to succeed compared to my age, now whosoever is jealousy out there should know that I am getting better every other day,”aliandika.

“I am sitted on my balcony uphill Seguku where the Leone Island come from. Watching museveni’s convoy pass by. I am not in debt with any bank as you wish be.”

Swali ni nani aliyekuwa akimpa dongo hilo? Bebe Cool ama Bobi Wine?

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wake walimkosoa msanii huyo kwa English yake ‘mbofumbofu’ambao aliwajibu, “all those correcting my English, put the blame on this damn iphone that spells before I ask it to. English is my 4th language but am happy to have you English teachers. Lord have mercy!!!!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents