Burudani

Juma Nature: Nataka nimalize kabisa na Yemi Alade

Msanii mkongwe wa muziki nchini Juma Nature, amesema anaupenda muziki wa msanii wa kike wa Nigeria Yemi Alade, hivyo anajipanga aingie nae studio ili waandae wimbo wa pamoja.
Juma Nature na Yemi Alade

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, Nature alisema anamkubali sana msanii huyo kutoka Nigeria, ambaye ameimba wimbo ‘Nagode’ kwa lugha ya kiswahili.

“Nataka nimalize kabisa na Yemi Alade, yeye ni msanii ambaye anaweza sana Afrika, anajua muziki kinyama, nikikaa nyumbani na kusikiliza madude yake, huyu dem Alade sio mtu mzuri, ujanja wangu wote yule kiboko, sijapata contacts ila najua nitazipata”, alisema Juma Nature.

Juma Nature amesema pia mwanamke huyo anajua anachokifanya ndio sababu anafikiria kumshirikisha kwenye kazi zake mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents