Burudani

Jux: Fiesta imeniwezesha kugundua nina ‘fanbase’ kubwa Tanzania

Kwa miaka mingi Jux amekuwa akiachia muziki tu unaofanya vizuri na kushindwa kuzunguka kwenye mikoa mingi nchini kutumbuiza kutokana na kubanwa na masomo, lakini kupitia Fiesta, muimbaji huyo amesema amegundua kuwa ana mashabiki wengi kuliko alivyotarajia.

14026801_283466592009621_2051747763_n

Ameiambia Bongo5 kuwa, kote ambako show hiyo imepita, amekuwa akiwaacha mashabiki wakitaka zaidi kutoka kwake.

“Nimegundua kwamba nina fanbase kubwa sana Tanzania hata sehemu zingine nilizokuwa nahisi labda bado, nimejua baada ya Fiesta,” amesema Jux.

“Nimegundua kwamba muziki unasafiri sana, watu wamefurahi hata mimi nimefurahi kwasababu mikoa mingi nilikuwa sijawahi kwenda kama Shinyanga, Muleba nilikuwa sijawahi kwenda, Singida pia sijawahi kwenda naenda sasa hivi,” ameongeza.

Jux anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Wivu’ ameongeza kuwa ameweza pia kugundua jinsi muziki wa Tanzania ulivyokuwa na ukubwa wa kushangaza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents