Habari

Kamanda Sirro kula saani moja na wauza CD zenye viashiria vya ugaidi

Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amewatahadharisha wafanyabiashara wa CD ambazo zina viashiria vya ugaidi kuacha mara moja biashara hiyo vinginevyo hatua kali zitachuliwa dhidi yao.

Akiongea na waandishi wa habari Jumamosi iliyopita Jijini Dar es salaam, alisema kama wasipotii amri hiyo ya kuacha kuuza CD hizo zenye viashiria vya ugaidi ndani yake basi Jeshi la Polisi litaanzisha msako mkali dhidi yao na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

“Hizi CD zina viashiria ambavyo vinahamasisha watu kufanya uhalifu kama ujambazi na masuala ya ugaidi, natoa angalizo kwa wafanyabiashara hao kuziteketeza, hii ni kwa ajili tu ya kuliweka Jiji letu katika hali ya usalama zaidi,”amesema Sirro.

Aidha, katika hatua nyingine, Sirro amewataka wafanyabishara wote wa CD wanaotandaza kando kando ya barabara kuacha mara moja kwani siyo sehemu sahihi na salama ya kufanyia biashara hiyo.

Hata hivyo, amesema kuwa hatua mbali mbali zinaendelea kuchukuliwa za kuhakikisha Jiji linakuwa salama na shwari, pia ametoa wito kwa wazazi, walezi, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla kufuatilia nyendo za watoto wao ili wajue wanajishughulisha na nini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents