Habari

Kampeni ya “Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto” kuwafikia watu 1000 Morogoro

Kampeni ya uelimishaji juu ya unywaji kiistarabu inayolenga kuwafikia wanafunzi wa vyuo,madereva, waendesha vyombo vya umma, na madereva bodaboda imeendelea huko mkoani Morogoro.


Kampeni hiyo ya siku mbili ijulikanayo kama “Usinywe na Kuendesha
Chombo cha Moto” itakayofanyika siku ya Jumamosi imelenga kuwafikia
watu 1000 kupitia maeneo mbalimbali ikiwamo sehemu za starehe ‘baa’,
vyuo pamoja na watumiaji wengine wa barabara.


Kampeni hiyo inayosimamiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) imeendelea na kimezinduliwa leo (juzi) Februari 23, 2019 katika Hoteli ya Nashera ambapo wadau mbalimbali wa usafirishaji ikiwamo Jeshi la Polisi,
Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) na madereva
walishiriki.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mkurugeni wa Uhusiano wa SBL,
John Wanyancha kampeni hiyo imelenga kuwafikia watu 1,000 wakazi wa
Mkoa huo ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika
kupunguza kiwango cha ajali za barabarani hapa nchini.


Mkurugenzi huyo alisema kampuni hiyo inashirikiana na wadau
mbalimbali ikiwmao Jeshi la Polisi-kitengo cha Usalama Barabarani
ambapo kampeni hiyo imekwisha kufanyika katika mikoa ya Mwanza na
Dar es Salaam mapema mwaka huu.


“Katika kampeni hii tunatoa vifaa mbalimbali vya uelimishaji ikiwamo
vipeperushi, vibandiko (stika), makoti ya usalama (reflectors), fulana
pamoja na kuwashirikisha wadau katika majadiliano yanayolenga katika
kutokomeza baadhi ya mila na desturi potofu juu ya matumizi ya pombe,”
alisema Wanyancha.


Aliongezaa “Unywaji kistaarabu hauishii tu katika kupunguza kiwango cha
pombe bali ni kutokuruhusu pombe itawale maisha yako au iongoze
mahusiano yako.”


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama
barabrani Mkoa wa Morogoro (RTO) Michael Deleli aliishukuru SBL kwa
jitihada hizo na kwamba kwa kulishirika Jeshi la Polisi ni chachu ya kuleta
mabadiliko chanya na kuzifanya barabara kuwa salama kwa watumiaji.


Hatahivyo, Deleli alisema anasikitishwa na vitendo vya baadhi ya madereva kunywa pombe kiholela pasipo kujali matokeo yake huku akitoa wito kuwatabia hizo zinatakwa kukoma ili kupunguza ajali zinazowza kuepukika.


“Jeshi la Polisi, madereva, watembea kwa miguu na makampui kama hii ya
Serengeti na jamii kwa ujumla tuna wajibu wakuhakikisha kuwa barabara
zetu zinakuwa salama kwa kuhamasisha madereva kuzingatia unywaji
kiistarabu,” alisema Deleli.


Aliongeza, “Nafarijika kuona kwamba licha kuwa ni Serengeti ni wazalishaji wa bia lakini wamejitoa kwaajili ya kupambana na tatizo la ulevi hasa kwa maadereva ambao wanabeba dhamana ya maisha ya watu wengi,” alisema Deleli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents