Habari

Mhe. Nape afunguka baada ya Mwigulu Nchemba kutumbuliwa ‘tuliolelewa humu ni kama mwanzi’

Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye ametoa kauli yake ya kwanza baada ya Rais Magufuli kutangaza kumtumbua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba

Nape amesema anamkaribisha Nchemba kwenye maisha ya kawaida ya ubunge ili kuanza majukumu yake ya kawaida ya kuwatumikia wananchi wake waliompa kura.

Cde Karibu Sana! Tuliolelewa humu ni kama Mwanzi, upepo ukivuma Mwanzi unalala, upepo ukiisha Mwanzi unasimama ukiwa imara zaidi! Tuwatumikie waliotupa kura!“ameandika Nape Nnaute kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mhe. Nape ni moja ya wabunge wa CCM waliowahi kuteuliwa na kutumbuliwa na Rais Magufuli katika kipindi kifupi cha mwaka 2015 hadi 2017.

SOMA ZAIDI – Nape Nnauye atumbuliwa, nafasi yake yachukuliwa na Dk. Mwakyembe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents