Michezo

Kila mtu Nchi hii anashabikia Liverpool – Guardiola atema cheche

Kocha wa Klabu ya Manchester City, Pep Guardiola ametoa madai yaliyowashangaza wengi baada ya kusema kwamba taifa zima linaikabili City kwenye mbio zake za kuwania Ubingwa wa Premier League.

Guardiola amedai kuwa taifa zima linataka Liverpool ishinda kombe hilo la Premier League.

”Kila mtu nchi hii anashabikia Liverpool, vyombo vya Habari na kila mmoja,” Guardiola amesema.

Pep Guardiola ameongeza ”Kwa sababu Liverpool ina historia ya kuvutia kwenye michuano ya Ulaya. Na sio Premier Leagues, kwa sababu imeshinda Ubingwa huu mara moja ndani ya miaka 30.”

”Lakini mimi sijali. Watu wanahitaji Liverpool ishinde zaidi yetu. Wanamashabiki zaidi Ulimwenguni na hapa England wanashabikia wengi zaidi yetu.”

Mabingwa hao watetezi watatwaa Ubingwa mara ya nne katika kipindi cha miaka mitano iwapo watashinda mechi zao tatu zilizosalia wakianzia na Wolves  siku ya Jumatano, huku Guardiola anaamini hilo lita huzunisha taifa.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button