Michezo

Kilichowakumba Man United chawakuta Simba SC, Timu daraja la pili yawakata mkia

Klabu ya Simba imevuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC) baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 dhidi ya Green Worriors inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.

Mchezo huo uliofanyika kunako dimba la Azam Complex, iliisha kwa sare ya mabao 1-1 ndani ya dakika 90 kabla ya kukutana kwenye hatua ya changamoto ya mikwaju ya penati.

Wachezaji watatu wa Simba, Muzamiru Yassin, Hussein Zimbwe ’Tshabalala’ na Jonas Mkude walikosa penalti zao kitu ambacho kiliizamisha klabu hiyo yenye kikosi ghari zaidi Tanzania.

Kipigo hicho cha kutupwa nje ya Kombe la Shirikisho kinakuja ikiwa ni siku mbili zimepita tangu klabu ya Manchester United itolewe kwenye kombe la EFL nchini Uingereza na klabu inayoshika mkia ligi daraja la kwanza ya Bristol City kwa kupigwa goli 2-1 .

Matokeo ya timu nyingine zilizofuzu hatua ya mzunguuko wa tatu wa kombe la shirikisho ni kama ifuatavyo;

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents