Michezo

Kilimanjaro Stars yaingia nusu fainali ya kombe la CECAFA

Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imetinga nusu fainali ya kombe la CECAFA kwa kuifunga timu ya Taifa ya Uganda ‘Uganda Cranes’ kwa penalti 3-2 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa Jumamosi hii nchini Kenya.

stars1

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa,timu zote zilitoka sare kwa kufungana mabao 2-2 ndani ya dakika 90, huku Uganda wakianza kuongoza kwa goli moja na baadae Mrisho Ngasa kuisawazishia Kilimanjaro na kuongeza bao la pili lililodumu hadi mapumziko.

Uganda walipata bao la kusawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare na timu hizo kwenda katika hatua ya mikwaju.

Kilimanjaro Stars ambayo ipo chini ya kocha Kim Poulsen walikosa penati mbili zilizopigwa na Erasto Nyoni na Mbwana Samatta, huku Uganda nao wakikosa penati mbili. Waliopata penati kwa upande wa Kilimanjaro ni Amri Kiemba, Athuman Iddi chuji na Kelvin Yondani.

Penati hizo ziliingia hatua ya pili huku Kipa wa Kilimanjaro Ivo Mapunda akiibeba Tanzania kwa kudaka penati ya hatua pili na kuifanya Tanzania kutinga katika hatua hiyo ya nusu fainali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents