Burudani

Kim Kardashian amkodishia Kanye West uwanja mzima Staples Center kucheza basketball na rafiki zake kama zawadi ya birthday

Kim Kardashian amempa mume wake zawadi ya birthday bora kabisa kuwahi kuitoa kwa mwanaume mwingine aliyewahi kuwa naye.

29765F0600000578-3116329-image-m-101_1433816454285

Kanye ametimiza umri wa miaka 38 Jumatatu hii.

Kim aliamua kukodisha uwanja mzima unaotumiwa na timu za kikapu za Los Angeles Lakers na L.A Clippers kwa siku nzima ili Yeezy aweze kucheza kipapu na washkaji zake.

2976123100000578-3116329-image-a-86_1433814950198

TMZ imedai kuwa Kim alilipa $110,000 kwaajili ya kukodi uwanja huo.

Kinachofurahisha zaidi ni washkaji aliocheza nao kikapu kwakuwa wote ni mastaa kuanzia nyota wa NBA Russell Westbrook na John Wall.

HakuwasahaU wanae, Justin Bieber, Tyga, na Pusha T. James Harden na 2 Chainz walikuwa makocha. John Salley alikuwa mtangazaji na John Legend akiimba wimbo wa taifa.

https://www.youtube.com/watch?v=4W9xxdbYrNo

Kim pia aliwalipa marefa halisi wa NBA kuchezesha mchezo huo na wasichana kadhaa wa Lakers wakitumika kumshangilia mumewe.

Pia Kobe Bryant, Magic Johnson, Carmelo Anthony, Shaquille O’Neal na Scottie Pippen walitengeneza video zilizochezwa kwenye screen za uwanjani hapo kumpongeza Kanye.

Unawezaje sasa kukataa kuwa hiyo ni zawadi ya birthday bora kabisa kwa mwaka huu?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents