Kingunge akanusha uvumi kuhusu kikao cha CCM Butiama

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ( NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru amewataka wananchi kuondoa fikra potofu kuwa safari yao ya Butiama ina lengo la kuomba radhi kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Na Patricia Kimelemeta


 


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ( NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru amewataka wananchi kuondoa fikra potofu kuwa safari yao ya Butiama ina lengo la kuomba radhi kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.


 


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Kingunge ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, alisema kikao hicho cha Butiama ni moja ya ziara ambazo halmashauri hiyo, imepanga.


 


Kingunge alisema kuwa, halmashauri hiyo, inaamua kwenda kufanya kikao katika mkoa wowote nchini , bila ya kuangalia ni wapi na kwa nani.


 


Alisema NEC imeamua kufanya vikao vyake Butiama kwa mujibu wa katiba na kwamba, wamepanga ykuzunguka kila mkoa ili kupanga mikakati yao pamoja na kuzungumza na wajumbe wa CCM kila Mkoa.


 


Aliongeza kuwa, watu wengi wamekuwa na tafsiri tofauti juu ya ziara hiyo, baadhi yao wanadai wanakwenda kuchukua baraka kwenye kabuli la baba wa Taifa wakati sio kweli, bali ni maamuzi yao kama viongozi wa NEC.


 


Kwa mujibu wa Kingunge, kazi ya halmashauri hiyo ni kutoa mapendekezo juu ya jambo ambalo chama hicho kinataka kufanya na kamati kutoa maamuzi .


 


Kikao cha NEC kinafanyika Machi 29 na 30 mwaka huu Butiama wilayani Musoma, Mkoa wa Mara.


 


Mambo mbalimbali kuhusiana na CCM yanatarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho cha siku mbili na kupanga mikakati juu ya utekelezaji wa chama chao.


 


Inatarajiwa kuwa, baadhi ya viongozi wa CCM watatangaza muafaka kati chama hicho na Chama cha Wananchi (CUF) visiwani Zanzibar, kuhusu mgogoro ya kisiasa uliodumu kwa muda mrefu.


 


Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents