Michezo

Klabu ya TP Mazebe yaandika waraka wa kulalamikia huduma mbovu walizopewa na Simba, wadai basi walilopewa liko chini ya kiwango, Haji Manara awajibu “Msitafute visingizio”

Klabu ya TP Mazembe ambayo iliwasili hapo jana usiku kwaajili ya kuwakabili Simba SC kwenye mchezo wao wa michuano ya CAF Champions league, wamejikuta wakilikataa basi lililoandaliwa na miamba hiyo ya soka Tanzania huku wakihusisha na maswala ya imani za kishirikina.

Mbali na kulalamikia basi hilo lakini pia wameenda mbali zaidi wakituma malalamiko ya kwa shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa kulalamikia huduma mbovu walizopewa na wageni wao.

Baada ya kuanza tuhuma hizo huku wakihusisha kwamba hata vilabu vingine vilivyocheza na Simba wakianza na Nkana kutoka Zambia, Alhly kutoka Misri, JS Soura kutoka Algeia na ndugu zao AS Vita kuwa walikutana na huduma hizo mbovu kutoka kwa Simba.

Ingawa Msemaji wa Simba Haji Manara ameamua kujijibu tuhuma hizo kwa kusema haya:-

Ikumbukwe Simba watacheza na TP Mazembe kutoka DR Congo siku ya Jumamosi katika uwanja wa taifa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents