Michezo

Klitschko kuzichapa na Anthony Joshua

Hatimaye bondia wa Uingereza Anthony Joshua na bondia wa Ukraine Wladmir Klitschko wamekubali kuzichapa huku tangazo la pigano hilo likitarajiwa kufanywa katika siku za hivi karibuni, kulingana na promota Eddie Hearn.

_91944418_joshuaklitschko

Pambano hilo la uzani mzito linafaa kuidhinishwa na mkatanda wa Joshua wa IBF mbali na mikanda ya WBA na WBO.

anthony_joshua-large_transqvzuuqpflyliwib6ntmjwfsvwez_ven7c6bhu2jjnt8
Anthony Joshua

Bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Tyson Fury alisalimu mataji yake ya WBO na WBA huku leseni yake ya kupigana ikifutiliwa mbali kwa muda.

Hata ivyo bodi ya Uingereza inayodhibiti leseni za mabondia ilimpokonya bondia huyo leseni yake kufuatia uchunguzi wa kutumia dawa za kusisimua misuli,baada ya bondia huyo mwenye umri wa miaka 28 kukiri kwamba amekuwa akitumia Cocaine ili kukabiliana na msongo wa mawazo.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents