Uncategorized

Koffi Olomide awasili Dar tayari kwa show kesho

Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide amewasili usiku wa kuamkia leo na kulakiwa na baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki usiku huo mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Mara baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo, Koffi Olomide alikwenda moja kwa moja kupumzika kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar tayari kabisa kwa shoo kali siku ya kesho. Mwanamuziki huyo machachari kutoka DRC Congo ameahidi kufanya shoo kali siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Leaders Club,Kinondoni akiwataka watanzania kuchagua nyimbo 15 wanazozipenda na yeye atawapa burudani kama ilivyozoeleka.

Shoo nyingine itakuwa siku ya jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= wenye tiketi na kwa shilingi 15,000/= getini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents