Habari

Korea Kaskazini yarusha makombora ya kwanza tangu 2017 na kuangukia karibu na pwani ya Japan, yadai wanafanya majaribio

Korea Kaskazini yarusha makombora ya kwanza tangu 2017 na kuangukia karibu na pwani ya Japan, yadai wanafanya majaribio

Korea Kaskazini imerusha makombora ya kwanza tangu 2017. Msururu wa makombora ya masafa mafupi yalirushwa Juammosi na kuangukia karibu na Bahari ya Japan.

Nordkorea Kim Jong Un in Pjöngjang (picture-allianvce/AP Photo/Korean Central News Agency)

Kwa mujibu wa DW Swahili, Korea Kaskazini imerusha makombora kadhaa ya masafa mafupi kutoka pwani yake ya mashariki Jumamosi, limesema jeshi la Korea Kusini. Wachambuzi wanasema Korea Kaskazini inaongeza shinikizo dhidi ya Marekani kwa kushindikana kupatikana makubaliano ya maana katika kutano wa kilele wa Febuari, Hanoi.

Jeshi la Korea Kusini awali lilisema yaliyorushwa ni makombora lakini baadae likashidwa kutoa maelezo zaidi.

Iwapo itathibitishwa kuwa ni uzinduzi wa makombora ya masafa mafupi basi yatakuwa ni ya kwanza kurushwa na Korea Kaskazini tangu uzinduzi wake wa mwezi Novemba 2017. Baada ya uzinduzi huo, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba uwezo wake wa kinyuklia umekamilika, na ikakubali kuanzisha tena mazungumzo na Marekani pamoja na Korea Kusini.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sarah Sanders amesem: “Tunanazo taarifa kuhusu hatua za Korea Kaskazini za usiku huu. Tutaendelea kuzifuatilia.”

Makombora ya Jumamosi ni ujumbe kwa Marekani

Korea Kusini imesema makombora hayo yalirushwa kutoka mji wa Wonsan wa Korea Kaskazini milango ya saa tatu asubuhi leo saa za Korea. Korea Kusini imeeleza kwamba inafanya uchunguzi kuhusu makombora hayo, ikishirikiana na Marekani.

USA-Nordkorea Gipfel - Donald Trump, Kim Jong Un (picture-alliance)Rais Donald Trump na Kim Jong-un walipokutana Hanoi, Vietnam, Alhamisi Febuari 28.2019

Waziri wa Ulinzi wa Japan amesema makobora hayo yameanguka karibu na pwani na nchi hiyo, na kwamba Japan haiko katiko kitisho chochote cha usalama.

Ijumaa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha alisema Korea Kaskazini inalazimika kuonyesha “hatua za uhakika” za kusitisha shughuli zake za kinyuklia iwapo inataka kuondolewa vikwazo ilivyowekewa.

Mapema wiki hii, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui ameonya juu ya matokeo yasiyofurahisha iwapo Marekani haitobadilisha msimamo wake kuhusu vikwazo vya kiuchumi ilivyoiwekea nchi yake.

“Hatua hii inaonyesha wazi kwamba Korea Kaskazini imekasirishwa na msimamo wa Marekani wa kuishinikiza nchi hiyo kusimamisha mpango wake wa kinyuklia lakini bila ya kuikubalia kuiondolea vikwazi ilivyoiwekea,” amesema Harry Kazianis wa gazeti la Marekani la masuala ya kimataifa la The National Interest.

Wachambuzi wanasema haijalishi ni makombora ya aina gani yaliyorushwa, ujumbe uliokusudiwa na KoreaKaskazini bila shak umeshaifikia Marekani.

Viongozi wa nchi hizo mbili Kim Jong-Un na Donald Trump wameshakutana mara mbili katika mikutano ya kilele lakini wameshindwa kufikia makubaliano.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents