Kulazwa hospitali kwa Nelson Mandela kwazua wasiwasi Afrika Kusini

Kulazwa hospitali kwa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela kumewaacha watu wake wa karibu gizani.

Msemaji wa Nelson Mandela Foundation Sello Hatang ameviambia vyombo vya habari kuwa hana taarifa za kulazwa kwa Mandela mjini Pretoria jana.

Naye mke wa zamani wa Mandela Winnie Madikizela-Mandela, amesema hakuwa na taarifa kuhusiana na kupelekwa hospitali kwa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini.

Ikulu ya Afrika Kusini inatarajia kutoa taarifa juu ya hali ya Mandela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents