Habari

Marquez amtwanga Pacquiao kwa knock out

Bondia Juan Manuel Marquez usiku wa kuamkia leo amemtwanga mfilipino Manny Pacquiao kwa knock out ya nguvu katika raundi ya 6.

Hiyo ni mara ya nne mabondia hao wanazichapa.

Pacquiao alikuwa amezidiwa katika raundi tatu za kwanza kabla ya kumdondosha Marquez chini katika raundi ya 5 lakini mambo yaligeuka katika raundi ya 6 baada ya Marquez kumshushia mpinzani wake ngumi nzito iliyompeleka chini kama gunia la mkaa.

Konde hilo lilimfanya Pacquiao alale chini kwa dakika mbili kabla ya kunyanyuliwa na watu wa benchi lake.

Baada ya pambano hilo lililofanyika jijini Las Vegas, Pacquiao alipelekwa hospitali huku Marquez aliyekuwa akivuja damu nyingi usoni kuvunjika pua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents