Habari

Kuzungumza Kiswahili ni kudumisha utamaduni wetu- Salma Kikwete

Balozi wa Kiswahili nchini, na mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete amewataka Watanzania popote watakapokuwa duniani kujivunia na lugha hiyo.


Balozi wa lugha kiswahili hapa nchini, na mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete.

Mama Salma Kikwete ametoa ushauri huo wakati wa hotuba yake katika hafla ya utoaji wa tuzo ya kwanza inayotambua mchango wa watunzi na waandishi wa fasihi ya lugha ya Kiswahili ya Mabati Cornell ya fasihi ya kiafrika ambayo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wasomi wa lugha ya Kiswahili kutoka vyuo mbalimbali duniani.

“Kiswahili ndiyo lugha yetu na Kiswahili ndicho kilichotuletea ukombozi, na Kiswahili ndicho utamaduni wetu,” alisema. “Tukisimama mbele ya mataifa tunapozungumza lugha yetu tunakuwa hatuna unyonge tunajulikana kama tuna kwetu na tuna bara letu. Kwahiyo ni lazima tukomboke kifikra, tusirudi nyuma naomba turudi wakati ule wa wakoloni walisema kila kitu chetu ni cha kijinga, tamaduni zetu waliziita ni za kishenzi,” alisisitiza Mama Salma.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents