Michezo

Kwaheri Ansu Fati

Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania imesema inatarajia kumuuza mchezaji wake Ansu Fati mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anayekipiga kwa mkopo katika timu ya Brighton ya nchini England, atauzwa mwishoni mwa msimu huu kwenda timu watakayofikia nayo makubaliano.

Taarifa iliyotolewa katika kurasa za klabu ya Barcelona, ilisema kuwa wanatarajia kumuuza mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa hiyo ilisema watamuuza Ansu Fati baada ya baadhi ya timu kuonyesha nia ya kuitaka saini yake.

Imeongezwa kuwa waliamua kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo kwenda Brighton kuhakikisha anaongeza kiwango chake tangu mwaka jana.

“Tulimtoa Fati kwa mkopo kwenda Brighton lakini ameshindwa kupanda kiwango, hivyo tumefikia mwafaka wa kumuuza mwishoni mwa msimu huu”.

Fati amecheza mechi 15 katika kikosi cha Brighton na kufanikiwa kushinda mabao mawili pekee.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents