Michezo

Ligi ya Uingereza yaongoza kwa kuwa na wachezaji wengi kwenye kikosi cha FIFA, Wafahamu wachezaji hao na klabu zao

Ligi ya Uingereza yaongoza kwa kuwa na wachezaji wengi kwenye kikosi cha FIFA, Wafahamu wachezaji hao na klabu zao

Ligi ya Uingereza ina idadi kubwa ya wachezaji waliochaguliwa kuorodheshwa miongoni mwa kikosi bora cha Fifa cha wachezaji 11 katika kipindi cha miaka kumi. Wachezaji 21 kati ya 55 walioteuliwa wanacheza soka yao ya kulipwa nchini England huku ligi hiyo ya Premia ikimaliza utawala wa ligi ya la Liga .

Wachezaji saba wa klabu ya Liverpool walioshinda ubingwa wa Ulaya wwameorodheshwa miongoni mwa wale watakaowania nafasi hizo 11 za kikosi cha Fifa ijapokuwa Real Madrid na Barcelona wana wachezaji wengi zaidi.

Kikosi hicho cha wachezaji saba 11 kitafichuliwa katika tuzo bora za Fifa mjini Milan tarehe 23 Septemba.

Zaidi ya wachezaji 23,000 wa kulipwa duniani walitakiwa kuchagua kikosi bora na Fifpro, Muungano wa wachezaji kutokana na kiwango cha mchezo wao kati ya tarehe 18 Julai 2018 na Julai 2019.

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio ManeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kikosi cha wachezaji 11 kitakachochaguliwa kitashirikisha mlinda lango, mabeki wanne, viungo wa kati watatu na washambuliaji watatu.

Wachezaji wanne wa Liverpool ni miongoni mwa wachezaji 17 watakaoshiriki kwa mara ya kwanza akiwemo Trent Alexander-Arnold na Andrew Robertson, huku wachezaji maarufu kama vile Romelu Lukaku na David Silva wakikosa kura za kutosha kushiriki kwa mwaka wa pili mfululizo.

Huku Ligi ya Premia ilio na wachezaji 21 ikimaliza utawala wa ligi ya la li Liga yenye wachezaji 20 katika kipindi cha miaka 9 kama ligi yenye wachezaji bora mabingwa wa Uhispania barceona ndiuo klabu ilioshirikishwa na wachezaji wengi zaidi.

Mshambuliaji wa Juventus Christiano Ronaldo

Wachezaji tisa wa klabu ya Barcelona walioshiriki katika kombe la mabingwa walishirikishwa huku Real Madrid ikiwa na wachezaji wanane, nayo Liverpool na Man City zote zikiwa na wachezaji saba.

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid ambaye alihamia Juventus Christiano Ronaldo ndiye mchezaji wa pekee kutangazwa katika orodha zote 11 za kikosi bora cha Fifa.

Kikosi bora cha Fifa duniani

Walinda lango: Alisson Becker (Liverpool), David De Gea (Manchester United), Ederson Moraes (Manchester City), Jan Oblak (Atletico Madrid), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona)

MabekiJordi Alba (Barcelona), Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Daniel Alves (Paris St-Germain/Sao Paulo), Joao Cancelo (Juventus/Manchester City), Daniel Carvajal (Real Madrid), Giorgio Chiellini (Juventus), Virgil van Dijk (Liverpool), Diego Godin (Atletico/Inter Milan), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Kalidou Koulibaly (Napoli), Aymeric Laporte (Manchester City), Matthijs de Ligt (Ajax/Juventus), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Andrew Robertson (Liverpool), Alex Sandro (Juventus), Thiago Silva (Paris St-Germain), Raphael Varane (Real Madrid), Marcelo (Real Madrid), Kyle Walker (Manchester City)

Viungo wa kati: Sergio Busquets (Barcelona), Casemiro (Real Madrid), Kevin de Bruyne (Manchester City), Christian Eriksen (Tottenham Hotspur), Frenkie de Jong (Ajax/Barcelona), Eden Hazard (Chelsea/Real Madrid), N’Golo Kante (Chelsea), Toni Kroos (Real Madrid), Arthur Melo (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Paul Pogba (Manchester United), Ivan Rakitic (Barcelona), Bernardo Silva (Manchester City), Dusan Tadic (Ajax), Arturo Vidal (Barcelona)

Washambuliaji: Sergio Aguero (Manchester City), Karim Benzema (Real Madrid), Roberto Firmino (Liverpool), Antoine Griezmann (Atletico/Barcelona), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Sadio Mane (Liverpool), Kylian Mbappe (Paris St-Germain), Lionel Messi (Barcelona), Neymar (Paris St-Germain), Cristiano Ronaldo (Juventus), Mohammed Salah (Liverpool), Son Heung-min (Tottenham Hotspur), Raheem Sterling (Manchester City), Luis Suarez (Barcelona)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents