Burudani

Lil Wayne atishia kuondoka YMCMB, awalaumu kwa kuzuia kutoa album yake

Lil Wayne ameishutumu label yake ya Young Money (YMCMB) kwa kuzuia kutoa album yake ya ‘Tha Carter V’ na kutishia kuondoka kwenye label hiyo.

lil wayne

Weezy ameandika tweet kama mvua za kulalamika,

“Kwa mashabiki wangu wote, nataka wote mjue kwamba album yangu haitatoka na haijatoka kwasababu Baby (Bird Man) na Cash Money Rec wamekataa kuitoa”.

Aliandika tweet nyingine,

“Hili sio kosa langu, naombeni sana mniwie radhi mashabiki wangu lakini zaidi kwangu mimi mwenyewe na familia yangu kwa kutuweka kwenye hali hii”.

Katika tweet nyingine Weezy alitishia kuondoka kwenye label hiyo,

“Nataka kuondoka kwenye label hii na sitaki kufanya chochote na hawa watu lakini bahati mbaya hiyo sio rahisi”

Na katika tweet nyingine aliongeza kuwa yeye amekuwa mfungwa pamoja na ubunifu wake.

tweet-1
tweet2

Hivi karibuni rapper Tyga naye alitumia Twitter kuilaumu Young Money kwa kuchelewesha kutoa album yake na kusema wamemuweka mateka.

Hata hivyo mkataba wa Weezy na Young Money aliosaini April, 2012 bado unamdai album nyingine tatu za kutoa chini ya label hiyo kabla hajawa huru kuondoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents