Burudani

Linah asaini mkataba mrefu wa usimamizi na Panamusiq inayomsimamia Ben Pol

Muimbaji Linah Sanga a.k.a ndege mnana amepata management mpya, ikiwa ni kipindi kifupi toka alambe deal la kuwa balozi wa Jebel.

Linah Pana

Linah ambaye hivi karibuni alikuwa Afrika Kusini kushoot video ya wimbo wake mpya, amesaini mkataba mrefu wa usimamizi na kampuni ambayo pia inamsimamia Ben Pol, Panamusiq Ltd.

“Panamusiq strikes another high profile deal by signing Linah on a long term
management contract. Linah is a Tanzanian award winning singer and performer with few hits in her catalogue including Ole Themba, Hellow . Christian Bell and Kizaizai ft. Diamond.”
yalisema maelezo ya Kampuni hiyo.

Linah amekuwa msanii wa pili kujiunga na kampuni hiyo baada ya Ben Pol. Kabla ya kujiunga na Panamusiq alikuwa akisimamiwa na kampuni ya No Fake Zone.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents