Burudani

Ongezeko la Ma-director wa video limepunguza kisingizio cha wasanii kushindwa kufanya video kwasababu ya uchache wao

Hivi sasa wasanii wa Tanzania hawana tena ‘excuse’ ya kushindwa kufanya video kwa kisingizio kilichokuwa kikitumiwa miaka ya nyuma, cha uchache wa ma-director.

Red

Miaka ya nyuma msanii alikuwa anaweza kushoot video leo na kuja kukabidhiwa kazi yake baada ya miezi mitatu, hii ilitokana na uchache wa ma-director waliokuwepo hivyo kila msanii alikuwa anawategemea wao. Lakini sasa msanii anaweza kushoot na kukabidhiwa video kwa muda mfupi zaidi hadi siku tatu.

Hivi sasa unaweza kutazama TV na kukutana na video nyingi ambazo zimefanywa na ma-director ambao wakati mwingine majina yao ni mageni kabisa kwenye masikio ya wengi.

Ben-Pol-2

Bongo5 imezungumza na Ben Pol ambaye kwa miaka mitano aliyokuwepo kwenye game ameshafanya kazi na ma-director wakongwe na wapya.

“Wasanii tulikuwa tunaweza tukasema kwamba labda nimeshindwa kufanya video kwasababu ya gharama, unajua tena unakuta kipindi hicho directors wakubwa wawili au mmoja lakini sasa hivi directors wako wengi mno na hata gharama zao unakuta tofauti kabisa.” alisema Ben Pol.

“unaweza kufanya video na director wa bajeti yako na video ikawa ni nzuri, ile sababu ya kusema nimeshindwa kushoot sababu sina hela inakuwa imekufa automatically, manake ni kwamba huwezi kusema nimeshindwa kufanya video kwa sababu ya hela kwasababu directors wapo na director wa bajeti yako yupo pia.” aliongeza Ben Pol.

Ben Pol pia amesema kuwa ushindani uliopo sasa kwa upande wa ma-director unawafaidisha zaidi wasanii kupata kitu bora zaidi.

“Ushindani pia umeongezeka kwa directors, speaking of ushindani ndo kitu ambacho sisi wasanii tunapenda kila siku tukione kwa directors, kwa sababu wanaposhindana wanaboresha kazi zao na wanavyoboresha wanatuboreshea pia na sisi video zetu kushoot. Kwahiyo tunakuwa tunapata video nzuri zenye standard kubwa.”

Ben Pol ameshafanya video na ma-director tofauti akiwemo mkongwe Adam Juma, Nisher na video yake mpya ya ‘Sophia’ amefanya na Khalfani na Hanscana ambao ni miongoni mwa madirector wapya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents