Habari

Lori laua watu Njombe

Watu wawili akiwemo Dereva wa Lori wamefariki dunia baada ya gari hilo kupinduka katika eneo la Lihogosa lililopo Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoid Banga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo April 19, 2024.

Kamanda Banga amesema chanzo cha ajali hiyo ni lori lilikwaruzana na Lori lingine la makaa ya mawe likiwa linatokea Makambako kuelekea Songea na kisha Kupinduka.

“Dereva wa Lori la mbao alipoteza maisha papo halo pamoja na mmiliki wa mzigo wa mbao lakini utingo wa lori ni majeruhi na amelazwa Hospitali ya Rufaa ya  Njombe, amesema Banga.

“Mpaka sasa dereva wa lori la makaa ya mawe hajakamatwa ili ahojiwe kuhusu ajali hiyo,” ameongeza Kamanda Banga.

 

Waliofariki dunia ni Dereva wa lori hilo Bryson Kihombo (30) na Juma Joseph (43) mmiliki wa mzigo wa mbao ambazo zilikuwa zikisafirishwa kuelekea Jijini Dar es Salaam.

 

 

 

 

 

 

 

 

CC:Tanzaniaweb.Live

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents