Habari

Mahakama yaitupilia mbali kesi ya kuzaa na mke wa mtu iliyokuwa ikimkabili Josephat Mwingira

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia  mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dkt. William Morris, raia wa Marekani dhidi ya mkewe Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha Ministry  na kutaka alipe gharama alizotumia mdaiwa.

Dkt. William Morris aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba mkewe, Mwingira na mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha kujua vinasaba  vya mtoto (DNA).

Dkt. Morris ambaye ni mume wa (mdaiwa wa pili, Phills Nyimbi) aliiomba mahakama itoe amri ya mkewe, Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA ili aweze kujua wazazi  halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.

Alidai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa huyo wa kiume.

Akisoma hukumu hiyo leo Februari 26,  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, amesema Dkt.  Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuonyesha mahusiano ya kimapenzi  kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.

Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na mke wa  Morris ni matokeo ya  mahusiano ya kimapenzi  kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents