Habari

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar azindua Monyesho ya miaka 60 ya Muungano Dsm

Katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanikiwa kusimamia utekelezaji wa masuala ya Muungano kwa ufanisi mkubwa kwa kuimarika kwa utaifa, umoja, amani, utulivu na hali ya maisha ya wananchi kutokana na ukuaji wa uchumi wa pande zote mbili za Muungano.

Ameyasema hayo Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibari Hemed Sulemani Abdulla Wakati akifungua Maonyesho Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika Viwanja vya mnazo Mmoja Jijini Dar es saalam Aprili 19,2024 amesema Taasisi za Muungano zimekuwa na ufanisi katika kuhakikisha usawa wa utoaji wa huduma kwa wananchi wa pande zote mbili kwani zimefungua Ofisi Tanzania Bara na Zanzibar ambao hadi sasa, Taasisi 33 zimefungua Ofisi Zanzibar kati ya Taasisi 39 za Muungano hivyo ni hatua kubwa katika kuimarisha huduma kwa wananchi wetu na kuimarisha Muungano.

Makamu wa Rais amebainisha kuwa kuwepo kwa Muungano kumesaidia sana kuimarisha hali za wananchi na kuinua uchumi wa pande zote mbili za hali hiyo imetokana kwa kuwepo kwa soko la pamoja lisilokuwa na vikwazo vya kiutawala na kiuendeshaji linalojumuisha ushirikiano na utengamano unaorahisisha mtiririko wa rasilimali na bidhaa, mitaji, watu na huduma baina ya Tanzania Bara na Zanzibar hivyo zipo fursa nyingi sana za kibiashara ambapo wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanaweza kuwekeza pande zote mbili za Muungano katika sekta za viwanda, hoteli na kujenga nyumba za biashara na makazi.

“Kwa upande wa kijamii, mafanikio makubwa yamepatikana katika miaka 60 ya Muungano kwani huduma za jamii zimeimarika hususani katika sekta ya afya, maji, elimu, ustawi na maendeleo ya jamii na makazi. Fursa za kijamii na utamaduni ni nyingi na zinazogusa mtu mmoja mmoja, vikundi na au taasisi. Udugu wa damu umeimarika sana kwani wananchi wa pande mbili za Muungano wameungana katika misingi ya ndoa na urafiki uliojengeka na kuimarika hali hii imechangia katika kupunguza migawanyiko ya kijamii na kuondoa hisia za ukabila na ubaguzi miongoni mwetu” amesema Makamu

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Hamza Khamis amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeendelea kuchukua hatua madhubuti za kutafutia ufumbuzi wa changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa masuala ya Muungano. Kuanzia mwaka 2006 hadi 2024, hoja 25 zilipokelewa na kujadiliwa ambapo kati ya hoja hizo, hoja 22 zimepatiwa ufumbuzi na kuondolewa kwenye orodha ya hoja za Muungano hivyo hoja zilizobaki zipo katika hatua mbalimbali za kupatiwa ufumbuzi na ni Imani yangu kuwa, kwa utashi na dhamira ya dhati ya pande zote mbili, hoja zilizobaki zitapatiwa ufumbuzi.

“Katika kipindi cha miaka mitatu, 2021 hadi 2024 hoja 15 zimepatiwa ufumbuzi kati ya hoja 18 zilizokuwepo. Utatuzi wa changamoto za Muungano umeongeza imani ya Watanzania kwa Serikali zetu na hivyo kuimarisha, kudumisha amani ya muda mrefu na utulivu wa Tanzania ambao ni Tunu muhimu na fahari ya nchi yetu. Kwa namna na umuhimu wa kipekee, naomba nitoe shukrani zangu za dhati viongozi wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mhe Dr. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambao wameendeleza kwa vitendo Mawazo na fikra za waasisi wa Muungano”amesema Naibu

Kwa Upande wake Meneja ukuzaji Biashara Mamlaka ya Maendeleo na Biashara TANTRADE Mohamed Tajin amesema lengo la maonyesho hayo ya miaka 60 ya muungano ni hizi mbili na taasisi ziweze kushiriki kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma wanazozitoa ikiwemo Uhamiaji ,Benki kuu,Zima moto Rita

Pia Tantrade imeshiriki na Wananchi wnakaribishwa kutembelea ili kufahamu huduma wanazotoa ikiwemo ukuzaji biasbara ndani na nji ya nchi kupitia Maonyesho yanayofanyika kila mwaka na mwaka huu wanatarajia kufanyika Juni 28 hadi Julai 13,2024.

Aidha itakumbuka kuwa uzinduzi wa maonesho kama haya ulifanyika Zanzibar tarehe 14 Aprili, 2024 na Rais Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi kwa hotuba yake ambapo aliweka wazi umuhimu wa Muungano wetu na fursa tulizonazo sisi wananchi wa pande zote mbili za Muungano na leo tena umezinduliwa hapa Dar es salaam Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hivyo kwaa hakika utamaduni huu ni kielelezo tosha ya mshikamano na uhusiano mzuri baina ya pandembili ili kuendelea kudumisha Muungano wetu adhimu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents