Habari

Makonda aitwa kujieleza Bungeni

Bunge limepitisha kwa kauli moja, azimio la kuitwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti ili kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.

Azimio hilo lililopitishwa Jumanne hii limetokana na hoja iliyowasilishwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara akisema wateule hao wa Rais wametoa kauli zinazodhalilisha hadhi ya mhimili huo wa Dola.

Akijibu swali kuhusu tuhuma dhidi yake zilizoibuliwa na wabunge kuhusu chanzo cha mali zake, Makonda aliwaambia waandishi wa habari kuwa wakati mwingine watunga sheria hao hulala bungeni kwa kukosa cha kuzungumza.

Wakati Mbunge Zitto Kabwe akipendekeza kuitwa mbele ya kamati viongozi waliotuhumiwa, Ester Bulaya amepasua jipu kwa kusoma ujumbe wa vitisho aliodai umetoka kwa kiongozi mmoja aliyeteuliwa na Rais.

Akichangia mjadala huo, Waziri anayehusika na Bunge pamoja na Sera Mh. Jenista Mhagama amewataka wabunge kutomuhusisha Rais Magufuli na makosa yanayofanywa na viongozi aliowateua ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria Rais ana majukumu yake, na wakuu wa mikoa na wilaya wana wajibu wao, hivyo kama kuna RC au DC anakwenda kinyume na sheria au kuingilia Bunge, anapaswa kuwajibishwa mwenyewe bila kumhusisha Rais.

Baada ya mjadala huo, Chenge amewahoji wabunge wanaokubaliana na mapendekezo ya mtoa hoja, ambapo wabunge wote wameitikia kuunga mkono mapendekezo hayo manne na kuwa maazimio rasmi ya Bunge.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents