Tragedy

Malkia wa Mipasho Khadija Kopa afiwa na mume wake

Malkia wa mipasho Tanzania na muimbaji ya TOT, Khadija Omari Kopa amefiwa na mume wake aitwaye Jaffari Ally usiku wa kuamkia leo (June 6).

khadija kopa1

Akizungumza na Bongo5 asubuhi hii mdogo wa marehemu aitwaye Aban Juma amethibitisha taarifa hizo na kusema marehemu amefariki saa 7:10 usiku wa kuamkia leo (June 6) katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam.

Kusuhu sababu za kifo chake Juma amesema marehemu alianza kusumbuliwa na kifua pamoja na kukosa pumzi siku kadhaa zilizopita, lakini hali ilizidi kuwa mbaya siku ya Ijumaa ndipo waliamua kumpeleka hospitali ya Lugalo siku ya Jumatatu (June 3).

Vipimo alivyochukuliwa katika hospitali ya Lugalo vilionyesha hana tatizo lolote, na hivyo walilazimika kuchukua vipimo vingine TMJ ambavyo mpaka mauti yanamkuta majibu yalikuwa bado hayajatoka kujua kilichokuwa kinamsumbua.

Khadija Kopa ambaye hakuwepo wakati mumewe anafariki anatarajiwa kurejea leo kutoka mkoani Rukwa alikokuwa ameenda kikazi, na msiba uko nyumbani kwao Bagamoyo.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema, Amen.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents