BurudaniVideos

Man Fongo hawezi kuandika nyimbo zake mwenyewe – Sholo Mwamba

Vita ya maneno ya kati ya wakali wawili wa Muziki wa Singeli, Sholo Mwamba na Man Fongo imezidi kupamba moto baada ya Sholo kuibuka na kudai kuwa Man Fongo hawezi kuandika nyimbo na hata kazi zake anazotoa hana uhakika kwa sababu ushauri mkubwa alikua anautoa kwake.

“Kwa sababu kama Man Fongo ni mtu mmoja ambaye kuandika hajui kwa maana hiyo kuna mtu mmoja anaitwa Mjani Maika huyo ndio mtu wake anamtegemea amuandikie muziki. Kwa maana hiyo akishapata kwa Mjani Maika yeye ndio anaenda kurekodi, ndio maana hata kuna kazi ameshirikishwa na Shishi hajafanya vizuri kutokana na mazingira yake ameshazoea kuandikiwa andikiwa,” alisema Sholo Mwamba nilipopiga naye story maskani kwao Shekilango.

Vita hii ya maneno kati ya wawili hawa imekuwa kama ni muendelezo wa pale ilipoishia. Hapo nyuma Man Fongo alimtuhumu Sholo kuwa alimzungumzia vibaya kwa Mama Wema kitu ambacho Sholo mwenyewe alikana nilipomuuliza.

Sholo kwa sasa anafanya kazi zake akiwa chini ya Muna Logistic inayomilikiwa na mwanadada Munalove. Ili kujua alichojibu Man Fongo baada ya maneno hayo ya Sholo mwamba endelea kutembelea Bongo5.com.

NA EDWARD FABIAN

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents