Michezo

Manchester City yaikomalia Arsenal kwa Arteta, Boss wa Tottenham adai hatishwi na timu za EnglandĀ 

Manchester City wanataka walipwe pauni milioni moja ili wavunje mkataba na kocha wao msaidizi Mikel Arteta – Arsenal wanataka kumtangaza Arteta kama kocha wao mpya. (Mail)

Image result for Mikel arteta

Liverpool wanatarajiwa kutupilia mbali mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 23, baada ya kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Japani na klabu ya Red Bull Salzburgforward Takumi Minamino, 24. (Star)

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amedai kuwa Spurs “hawaogopi” kumuuza kiungo mchezeshaji raia wa Denmark Christian Eriksen, 27, kwa timu pinzani za England mwezi ujao. (Evening Standard)Christian Eriksen

Je, hatimaye Eriksen kuihama Spurs Januari?

Kampuni Tajiri kutoka Abu Dhabi, Falme za Kiarabu ambayo inataka kuinunua klabu ya Charlton Athletic imehojiwa na bodi ya Ligi ya Premier juu ya mahusiano yake na wamiliki wa klabu ya Manchester City ambao pia wanatokea Abu Dhabi. (Telegraph)

Carlo Ancelotti anatarajiwa kutangazwa kama kocha mpya wa Everton baada ya kusaini mkataba wa pauni milioni 11.5 kwa mwaka. (Mirror)Ancelotti

Ancelotti hivi kariuni ametimuliwa Napoli licha ya kuifikisha klabu hiyo hatua ya mtoano Champions League

Juventus wanatarajiwa kumbakiza beki wao raia wa Uturuki Merih Demiral, 21, licha ya klabu kadhaa za ligi ya Primia na pia AC Milan kuonesha nia ya kutaka kumsajili. (Calciomercato)

Paris St-Germain wanatarajiwa kusuka mipango ya kumsajili Pep Guardiola kama mbadala wa kocha wao wa sasa Thomas Tuchel. (Le 10 Sport via Daily Mail)

Winga Mjerumani Leroy Sane, 23, anataka kuhamia nyumbani kwao Bayern Munich na anapiga hesabu za kuihama Manchester City mwezi Januari. (Bild via Mirror)Leroy Sane

Bayern Munich wamekuwa wakimtaka Leroy Sane kwa muda, na sasa yeye pia ameonesha nia ya kujiunga nao

Liverpool, Chelsea na Tottenham ni miongoni mwa vilabu ambavyo vinamnyemelea mshambuliaji kinda wa Nigeria anayechezea klabu ya Lille ya Ufaransa Victor Osimhen, 20. (Sky Sports)

Kiungo Mhispania Marcos Llorente, 24, anatakiwa na klabu kadhaa katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari lakini Atletico Madrid hawataki kumuuza. (AS – in Spanish)

Liverpool wanaendelea kumfuatilia beki wa kushoto wa klabu ya Toulouse ya Ufaransa Mathieu Goncalves, 18. (L’Equipe via Talksport)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents