Habari

Marekani: Spika wa Bunge aagiza rais Trump kuchunguzwa, adai lazima awajibishwe, hakuna mtu aliye juu ya sheria

Kwa miezi kadhaa Spika Pelosi amesita kufungua mashtaka ya kumuondoa madarakani Rais Trump kufuatia shutuma za awali za kuingilia kati sheria kuchukua mkondo wake kutoka kwenye ripoti ya Robert Mueller juu ya Russia kuingilia kati uchaguzi mkuu wa Marekani 2016.

Image result for Nancy Pelosi

Spika wa bunge la Marekani m-Democrat Nancy Pelosi ametangaza rasmi kuanzisha uchunguzi wa kutaka kumuondoa mamlakani Rais wa Marekani Donald Trump na shutuma kwamba aliiomba serikali ya nje kusaidia juhudi zake za kuchaguliwa tena kwenye uchaguzi mkuu Marekani 2020.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha ‘Voice of America’, Pelosi alitoa tangazo hilo baada ya kukutana ndani ya jengo la bunge na viongozi wa Democratic huku wabunge kadhaa wa chama hicho ambao wanaunga mkono kufunguliwa mashtaka ya kumuondoa madarakani Trump wameendelea kuongezeka kwa siku ya Jumanne.

Pelosi alisema “hatua zilizochukuliwa hadi hivi sasa na rais zimekiuka katiba ya nchi. Rais lazima awajibishwe. Hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria.”

Ujumbe wa Rais Trump akijitetea kupitia ujumbe wake wa Twitter kwa kile kinachozungumzwa dhidi yake katika mawasiliano aliyofanya na rais wa Ukrain.

Kwa miezi kadhaa Pelosi amesita kufungua rasmi mashtaka ya kumuondoa madarakani Rais Trump kufuatia shutuma za awali za kuingilia kati sheria kuchukua mkondo wake kutoka kwenye ripoti ya mwendesha mashtaka maalumu Robert Mueller juu ya Russia kuingilia kati uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016.

Lakini katika siku za karibuni shinikizo limeongezeka kwa Pelosi kufuatia ripoti kwamba Trump alimtaka Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kumchunguza mgombea urais wa Democratic na Makamu Rais wa zamani Joe Biden juu ya ajira yenye malipo ya juu aliyokuwa nayo mtoto wake wa kiume Hunter Biden katika kampuni moja ya gesi ya Ukraine.

Biden amekuwa mgombea anayeongoza kwa uteuzi wa urais kupitia Democratic na mpinzani anayeweza kumkabili Trump katika uchaguzi wa 2020.

Trump alisema atatoa Jumatano taarifa kamili ya maandishi iliyorekodiwa juu ya mazungumzo yake ya simu mwezi Julai na Rais Zelenskiy.

Lakini Pelosi na wa-Democratic wengine wanasema kuna mengi kwenye shutuma hii dhidi ya Trump zaidi ya mazungumzo ya simu.

Trump alithibitisha alimwambia mfanyakazi wake kuhodhi dola milioni 400 za msaada kwenda Ukraine siku kadhaa kabla ya mazungumzo ya simu ya mwezi Julai. Wa-Democratic wanataka kujua kama Trump alimshinikiza Zelenskiy kufanya uchunguzi kwa Biden, akijua fika kwamba serikali ya Ukraine inahitaji sana msaada wa Marekani. Alisema alizuia fedha hizo mpaka nchi nyingine ikiwemo zile za Ulaya pia zinatoa msaada kwa Ukraine.

Mzozo wa hivi sasa ulianza wiki iliyopita wakati ripoti zilipoibuka kwamba mtu ambaye hajatajwa jina kutoka timu ya ujasusi wa taifa ametoa siri za serikali na kuwa makini kuhusu mifululizo ya hatua ndani ya utawala wa Trump. Wanajumuisha kile hivi sasa kinachojulikana kuwa mazungumzo ya simu ya Trump na Zelenskiy.

Mtu huyu aliwasiliana na Inspekta Jenerali wa ujasusi ambaye aliyaita malalamiko hayo ni makubwa na ya dharura.

Lakini kaimu mkurugenzi wa idara ya taifa ya upelelezi Joseph Maguire amekataa kukabidhi ripoti ya Inspekta Jenerali kwa bunge ambapo sheria inamtaka kufanya hivyo.

Mwenyekiti wa kamati ya upelelezi bungeni Adam Schiff alisema Jumanne kwamba mwanasheria wa mtu aliyetoa siri za serikali alimfahamisha Schiff kwamba mtu huyo anataka kukutana na kamati. Schiff alisema kwamba mkutano utafanyika haraka iwezekanavyo wiki hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents