Burudani

Mastaa wa tamthilia ya Bones waishtaki Fox

Mastaa wa tamthilia ya ‘Bones’, Emily Deschanel na David Boreanaz wameungana na mtayarishaji mkuu, Barry Josephson kuishtaki tamthilia ya Fox kwa faida ambayo hawakulipwa.

1280x960_Bones_wallpaper_bb-skull

Waigizaji hao waliwasilisha malalamiko yao Jumatatu kwenye mahakama ya jijini Los Angeles pamoja na mwandishi na mtayarishaji mkuu, Kathy Reichs, wakidai kuwa kampuni ya 20th Century Fox iliwadhulumu mamilioni ya dola ya faida kwa kuficha nyaraka na kudanganya mahesabu.

Mashtaka hayo yanadai kuwa ukaguzi wa mahesabu umegundua kuwa walifichwa uwepo wa dola milioni 100 zilizoingizwa na tamthilia hiyo.

Reichs alidai kuahidiwa asilimia tano ya faida huku Deschanel na Boreanaz wakiahidiwa asilimia tatu kila mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents