Burudani

Mastaa waliokuwa marafiki na kugeuka maadui

Kuna baadhi ya mastaa Bongo waliofanikiwa kuwa marafiki wakubwa na kushare kila kitu wanachokifanya lakini mwisho wa siku mambo yakaenda kombo kwa urafiki wao kuanza kugeuka kuwa uadui.

Hawa ni mastaa waliokuwa marafiki lakini mwisho wamegeuka na kuwa maadui.

Diamond na Ommy Dimpoz

Ommy Dimpozi na Diamond  Baada ya show

Wawili hawa walikuwa karibu sana mpaka baadhi ya mashabiki walianza kuwaita mapacha kutokana na ukaribu wao. Muda mwingi walikuwa pamoja japo hawakuwahi kufanya collabo kwenye wimbo wowote zaidi ya kushirikishwa kwenye nyimbo mbili ‘Utamu’ ya Dully Sykes na ‘Prokoto’ ya Victoria Kimani.

Katika hali ya kushangaza mastaa hawa baada ya muda walionekana kuanza kuvimbiana huku wakikaushiana bila ya kusalimiana kwenye baadhi ya maeneo kadhaa waliokuwa wakikutana.

Mpaka sasa bado haijulikani chanzo cha ugomvi wao huku kila mmoja akiendelea kusema kuwa hana tatizo na mwenzake lakini mashabiki wengine wametengeneza vyanzo vyao kwa kudai kuwa chanzo cha ugomvi huo ni Dimpoz kuonekana kuwa karibu na Wema Sepetu ambaye alikuwa ex wa Diamond. Dimpoz alimtumia Wema kwenye video ya wimbo wake, Wanjera.

Wema Sepetu na Kajala

280KAJALA_WEMA

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. Hilo alilionyesha Wema Sepetu miaka kadhaa nyuma wakati hakimu alipotoa hukumu kwa Kajala kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka au kutoa faini ya shilingi milioni 13.

Mastaa hao walikuwa kama mapacha baada ya msala huo kumalizika mpaka ilifikia hatua Kajala alichora tattoo ya jina la Wema Sepetu kwenye mwili wake. Baada ya muda wawili hao walionekana kuanza kuwa maadui na kila mmoja alianza kumkashifu mwenzake kupitia timu yake ya mitandaoni.

Kila mmoja amekuwa akimtupia mpira kuwa ndiye chanzo cha ugomvi wao huku wengine wakidai kuwa chanzo cha matatizo hayo ni kigogo mmoja wa ikulu ndiye aliyewachanganya mashosti hao kwa kipindi kile. Lakini pia Wema amempoteza aliyekuwa rafiki yake mwingine wa karibu, Aunty Ezekiel huku chanzo cha matatizo yao yakiwa hayajulikani.

Young Dee na Mtu Chee

Mtu

Mtu Chee ni kundi lililokuwa linawahusisha wasanii watatu akiwemo Young Dee, Country Boy na Stamina.

Baada ya muda Young Dee aliamua kujitoa kwenye kundi hilo huku akidai kuwa haoni muendelezo wa kundi hilo kutokana na kukaa kwa muda mrefu bila ya kuachia wimbo hali iliyopelekea nafasi yake kuchukuliwa na rapa Young Killer japo hajawa member wa moja kwa moja ndani ya kundi hilo.

Hali hiyo imezua sintofahamu kadhaa kwa mashabiki kutokana na kauli zinazotolewa na wasanii hao wanapohojiwa akiwemo Stamina alipohojiwa na Jembe FM alisema, “Mimi ni mwanajeshi ambaye ni jeshi la mtu mmoja sifungamani na mtu na wala sitegemei usaidizi wa mtu mimi, mimi naweza nikasurvive mwenyewe na mambo yangu yakaenda vizuri tu. Kwahiyo kauli yake yeye arudi, asirudi sisi walaa, kwanza habari yake nimeiona Bongo5, nisingeiona walaa, kwanza simpigiagi simu, yaani sio mwana kiufupi,anajua mwenyewe mistake zake anazofanyaga.

“Kwasababu sasa hivi anaona amerudi sehemu ile ile, anarudi kwenye yale matapishi aliyokuwa amekula mara ya kwanza, ameona kuwa watu wamekubali kumsaidia tena it’s okay. Halafu mimi si selfish aisee, sababu huyu huyu siku kadhaa tu zilizopita tulikuwa tunaishi naye kitaa vizuri tu na tulikuwa na mipango ya kufanya naye kazi lakini mimi watu wenye dharau sio wanangu kabisa,” alisisitiza Stamina.

Natamani kuona siku baadhi ya mastaa waliogombana waje kupatana kwa sababu hakuna marefu yasiyo na ncha lakini inapaswa kukumbukwa kuwa hutakiwi kugombea fito wakati mlango upo. Ni furaha iliyoje kwa sasa Diamond na Wema Sepetu wameanza kuonekana kusamehana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents