Habari

Matokeo darasa la nne, kidato cha Pili yatangazwa

Barazala la Mitihani Tanzania (Nacte) limetangaza matokeo ya kidato cha pili na darasa la nne, jumla ya wanafunzi 1,320,700 kati ya 1, 592, 235 wenye matokeo sawa na asilimia 82.95 wamefaulu mitihani upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kwa kupata madaraja A, B, C D.

Kati yao wasichana ni 694, 547 sawa na asilimia 84.76 na wavulana ni 626,153 sawa na asilimia 81.03.

Wakati matokeo ya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili, uliofanyika Oktoba/Novemba 2022 ,ambapo jumla ya wanafunzi 539, 645 kati ya 633, 537 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 85.18 wamefaulu katika madaraja ya I, II, III na IV.

Kati yao wasichana ni 283,541 sawa na asilimia 83.05 huku wavulana wakiwa ni 256, 104 sawa na asilimia 87.67

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents