Burudani

Mayweather awapiga dongo 50 cent na McGregor baada ya ushindi wake dhidi ya Nasukawa

Pambano la Bondia wa Marekani Floyd Mayweather na ‘kickboxer’ mwenye umri wa miaka 20 Tenshin Nasukawa lililofanyika usiku wa kuamkia mwaka mpya limeweza kumuingizia Mayweather kiasi cha Dola milioni 9.

Pambano hilo limeingiza kiasi hicho cha fedha ndani ya dakika 2 tu alizozitumia Mayweather kupigana na Nasukawa ambapo Mayweather aliweza kushinda pambano hilo (KO).

Baada ya ushindi huo wa Floyd aliweza kuandika maneno mazito ambayo yanaonekana kama dongo kwa mtu fulani, lakini baada ya utafiti na uchunguzi kufanyika kwamba hilo dongo linamlenga nani, ikabainika kumbe linawalenga watu wawili ambao walikuwa na bifu nyuma.

Watu ambao Mayweather aliwalenga ni rapper 50 Cent pamoja na mpiganaji wa MMA ambaye kipindi cha nyuma alipigana na Mayweather na Mc kudundwa (KO) na Mc Gregor.

lakini lilipotangazwa pambano la Mayweather na Mjapan Nasukawa ndipo maneno yalipoanza, McGregor aliposikia pambano hili alisema hivi:-


”Hiyo ni ‘tracksuit’ au ‘sauna suit’ Floyd hahaha, hivi kuna habari gani hapa Tokyo ?, haya kweli ni mabadiliko ya hali ya hewa wala siyo masihara,”
 

na Mayweather kumjibu McGregor hivi:- ” Ujinga gani unaendelea hapa ?, ni nani huyu dogo unayekwenda kupigananaye ?, huu ni uwendawazimu,”
”Tunafanya mambo ya kijinga wakati mwingine, lakini mimi siyo miongoni mwao. Kama naiyona fursa ya kutengeneza dola milioni 300 (kama bilioni 686 za Tz) kwa sekunde kwa nini nisipigane,”

Mbali na bifu hilo la McGregor na Mayweather lakini pia Mayweather alikuwa na bifu kali sana na 50 Cent na bifu hili lilikuwa la kuringishiana zaidi pesa.

Baada ya pambano la jana McGregor na 50 Cent waliweza kumkejeli Mayweather kwa kupambana na mtoto mdogo naa Mayweather aliandika hivi:- ” What if I told you I was making $9,000,000 for 9 minutes of sparring in Tokyo Japan would you do the same if you were me? I like to call it a 9 minute walk thru.
#Tokyo
#Japan” Kitu ambacho nilikuambia kuwa nitatengeneza dola 9,000,000 kwa dakika 9 , Tokyo Japan, Je…? ungekuwa wewe ungefanya kama nilivyofanya mimi ? Napenda kuiita hii ni kutembea ndani ya dakika 9 Tokyo .”

Hayo Maneno yalionyesha kabisa yanamlenga McGregor kwani Mc aliandika hivi:-

Hizo milioni 9 haziwezi kukuweka juu katika orodha yangu”

Mbali na hayo maneno ya McGregor lakini pia 50 Cent ameandika hivi:-

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents