Habari

Mh. Mbowe aruhusiwa kutoka hospitali KCMC

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) ameruhusiwa kutoka hospitali hapo baada ya madaktari kujiridhisha kuwa afya yake imeimarika.

Mbowe alilazwa hospitalini hapo kuanzia juzi usiku ambapo alikuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa.

Ikumbukwe kuwa Mh. Mbowe alifikishwa KCMC Machi 4 akiumwa kichwa na jana Machi tano ameruhusiwa kutoka hospitalini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents