Habari

Mbunge CUF afunguka upinzani kususia kiapo cha wabunge wapya

Wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wamesema kuwa sababu ya wao kususia wabunge 7 wateule wa CUF kuapishwa wanapinga bunge kutumika na serikali.

Hayo yamezungumzwa leo na Katibu wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni, David Silinde kambi hiyo haitawapa ushirikiano wabunge hao mpaka kesi ya msingi itakapo malizika mahakamani.

“Sababu kubwa ya kutoingia tunapinga Bunge kutumika na serikali,kukandamiza upinzani, kutofuata sheria za nchi na jambo la tatu tunawaunga mkono wabunge walioondolewa na hatuintertain kuna vitu vikubwa ambavyo tumekuwa tukikasirika navyo serikali kuintertain chama ambacho kipo kwenye mgogoro kwamba unapendelea upande mmoja unaacha upande mwingine na hili ndilo tulilokuwa tukilisema siku zote hatutaki bunge kutumika,” alisema Silinde.

“Tunataka tuwe na bunge imara na tuige mifano iliyotokea kule Kenya Mahakama inaweza kusimama peke yake na tunataka bunge letu liendelee kusimama peke yake sio kuintertain upande mmoja kwahiyo tunaona udhaifu mkubwa katika bunge na tutaendelea kupinga siku zote tukiendelea kukaa hapa bungeni na hilo ndo jambo kubwa tunalotaka Watanzania wafahamu kwa siku ya leo.”

Kwa upande wake, Katibu wa Bunge wa Chama cha wananchi (CUF), Bwana Juma Kombo Hamad ameongea na Bongo5 kuwa lengo ni kuwaunga mkono wabunge waliofukuzwa, na kupinga kwa nguvu zote bunge kuingiliwa na muhimili wa serikali , huku akisema wanataka bunge huru na lenye kujitegemea na kwamba hawatatoa ushirikiano wowote kwa wabunge walioapishwa leo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents