Mexico: Watu 23 wafariki dunia baada ya barabara ya juu kuporomoka na treni kudondoka (+ Video)

Imeelezwa kuwa takriban watu 23 wamefariki dunia baada ya sehemu ya barabara ya juu kuporomoka na kusababisha treni ya abiria kuanguka katika barabara ya chini iliyokuwa na watu wengi.


Waokoaji walilazimika kushikilia sehemu ya treni hiyo kwa kreni ili kuwaokoa abiria waliokuwa wamekwama ndani ya kifusi. Watu 70 wamejeruhiwa na 49 kati yao wapo mahututi.

Barabara hiyo ya juu imewahi kulalamikiwa kwa kujengwa chini ya kiwango baada ya kukamilika kwake mwaka 2013.

Kwa uchache watu inaelezwa kuwa kati ya watu 49 mpaka 65 waliojeruhiwa walisafirishwa hospitalini, pamoja na saba ambao walikuwa katika hali mbaya na walifanyiwa upasuaji.

“Kwa bahati mbaya, kuna watoto kati ya waliokufa wapo” meya wa jiji la Mexico aliwaambia waandishi wa habari, bila kutaja ni wangapi.

Bofya haap chini kutazama.

 

https://www.instagram.com/tv/COdJlM-BeNn/

 

Related Articles

Back to top button