Habari

Mhe. Lema afunguka kuhusu matairi ya gari lake kufunguliwa

Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema amesema kuwa walibaini tairi za mbele za gari lake kufunguliwa baada ya wheelnut 13 kati ya 20 kufunguliwa bila kufahamika nini chanzo chake.

Mhe. Lema leo amezungumza na waandishi wa habari juu ya gari lake kufunguliwa wheel nut ambapo mke wake ndiye aliegundua baada ya kuhisi kama kuna kitu kinagonga kushoto kwa gari hilo.

“Kuhusu gari langu, gari langu leo lilipata accident ndogo yaani maana yake matairi yalifunguka na gari likalala chini siku tatu kama zilizopita, mimi nilikuwa nikisafiri kuelekea Moshi na mke wangu akasema na sikia kelele mguu wangu wa kushoto sasa jana wakati natoka nyumbani nilisikia kelele hiyo na niliamua kulipaki eneo la hoteli moja inaitwa Ikweta na nikaacha funguo, nikatoa maelekezo kwamba dereva akija anapaswa kulichukua alipeleke kwa fundi ajue lina tatizo gani, asubuhi wakati dereva analichukua gari ameondoka tu kidogo lile gari matairi yalifunguka likawa limekita chini sasa baada ya kuangalia walikuta zile wheelnut ina wheelnut 20,” alisema Mhe. Lema.

“Wheelnut 13 zilikuwa zimefunguliwa kulikuwa na wheelnut 7 peke yake, sasa niliongea na mke wangu yeye yupo Arusha nikamwambia aangalie kwenye camera nyumbani kwetu aangalie kwenye camera, Katibu wangu aandike barua apeleke polisi lakini vilevile mimi ntaandika barua polisi kupeleka kwa Mkurugenzi wa usalama wa Taifa na kupelekwa kwa DCI, kwasababu kuna tetesi tumekuwa tukizisikia kuna mambo mengi ya kupangiana njama na wengine wamesema hata shamba langu Kilolo Iringa wanataka kupanda bangi, siamini kwamba wheelnut 13 zinatoka kwa bahati mbaya zote, ndio maana nimesema waangalie nyumbani kwenye camera na kama ni bahati mbaya huyo mchawi atakuwa na degree za kutosha kwahiyo taarifa za awali ndio hio.” aliongeza Lema.

Hata hivyo Mbunge huyo asubuhi ya leo alitweet kama inavyoonekana hapo chini, hii ndio ilipelekwa waandishi wa habari kutaka kujua nini hasa kilichosibu kwenye gari la mbunge huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents