Michezo

Mo Dewji: Sijawahi kumuona Morrison live, namuonaga kwenye Tv tu na nilimwambia Simba kwanza nidhamu (+Video)

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mo Dewji amezungumzia tabia ya utovu wa nidhamu aliyokuwa nayo mchezaji wao mpya Bernard Morrison na nama watakavyokabiliana nayo ikiwa ni swali kutoka kwa Mwandishi wa Habari.

”Mimi sijawahi kukutana na Morrison, nimemuona kwenye TV ila ana kwa ana hatujakutana hata siku moja.” – amesema Mo Dewji.

Mo ameongeza ”Nimeongea naye kwenye simu nimemuambia kwamba hii klabu inaendeshwa kwa nidhamu, nimemuambia kwamba nenda kwenye Instagram yako andika waambie mashabiki wa Simba kwamba mimi nitakuwa na nidhamu.” ”Na mimi kaniahidi mwenyewe kwamba atakuwa na nidhamu. Hii Corona imetuvuruga sana tulikuwa tunataka yulete timu kubwa ije icheze na Simba.”

https://www.youtube.com/watch?v=2_1G-ot8tFw

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents