Michezo

Mourinho: Nitawaweka benchi baadhi ya wachezaji dhidi ya Arsenal

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa atawapumzisha baadhi ya wachezaji wake katika mechi ya siku ya Jumapili dhidi ya Arsenal.

Ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya klabu ya Uhispania Celta Vigo siku ya Alhamisi ulikuwa wa 10 tangu mwezi Aprili.

Huku kikosi hicho cha Mourinho kikiwa katika nafasi ya tano katika Msimamo wa ligi ya Uingereza, ligi ya kombe la Europa inaweza kuwapatia fursa ya kushiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao.

”Wachezaji ambao wameshiriki katika mechi nyingi hatawachezeshwa wikendi”, alisema Mourinho.

Mpira wa adhabu wa Marcus Rashford uliipatia United ushindi katika mchezo wakwanza  na nchini Uhispania huku mcezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa siku ya Alhamisi ijayo katika uwanja wa Old Trafford.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents