Michezo

Wanyama: Spurs mabingwa wa Uingereza msimu huu

Mchezaji wa klabu ya Tottenham, Victor Wanyama anaamini klabu yake inaweza kunyakua ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza msimu huu. Spurs wanaweza kupunguza pengo la alama baina yao na vinara wa ligi kuu, klabu ya Chelsea, kama watafanikiwa kuwafunga West Ham.

Wakati kikosi cha Meneja , Antonio Conte kikiwasubiri klabu ya Middlesbrough, mchezo utakaopigwa katika Dimba la Stanford Bridge, usiku wa Jumatatu. Mchezaji huyo ameliambia shirika la utangazaji la Sky Sport;

“Nadhani itakuwa na maana kubwa, Kuwafunga wapinzani wetu mbele ya mashabiki zetu,”
“Tunahitaji mafunzo na kituma zaidi ikiwa ni kama maandalizi ya mchezo wetu huo unaofuata. Lakini pia tunafahamu utakuwa mchezo mgumu.

“Tunachohitaji sisi ni kuwa makini na kubaki katika ubora tuliokuwa nao, tukijiwekeza zaidi huko tutatoka na matokeo mazuri. Na kujiona mbali.

“Tutafanya hivyo kila mchezo uliopo mbele yetu. Tutaendelea kuwa imara na tutamaliza tukiwa imara. Bila ya kujali nini kitatokea, tutakacho kifanya ni kujiwekea u makini na kuendelea na ubora tulio kuwa nao.
“Kama mchezaji wakati mwingine unashindwa kuona vitu vidogo. Ndio maana unahitaji kwenda mbali zaidi ili kuhakikisha unapambana na kuji hakikishia unapata mafanikio.

“Nahisi kuwa bora kilasiku na kuzidi kuwa na kiwango bora zaidi.
“Nalikuwa nafuraha kujiunga hapa.”

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents