Burudani

Mpenzi wa zamani wa Lil kim ‘Mr Papers’ ajitokeza na kudai kuwa ndiye baba wa mtoto mtarajiwa wa Kim

Taarifa juu ya ujauzito wa rapper wa kike wa Marekani Lil Kim zilifahamika wiki iliyopita kama surprise baada ya rapper huyo kuhudhuria New York Fashion Week akiwa na tumbo kubwa, lakini bado haikuwa wazi ni mwanaume gani ambaye anatarajiwa kuwa baba wa mtoto huyo mtarajiwa.

Lil Kim n baby daddy
Mr Papers na Lil Kim

Baada ya vyombo mbalimbali vya habari kuandika habari hiyo huku vikiacha swali la nani baba wa mtoto huyo mtarajiwa, ex boy friend wa Lil Kim ambaye pia ni rapper Mr Papers amejitokeza hadhari na kudai kuwa yeye ndiye baba mzazi mtarajiwa wa mtoto huyo mtarajiwa.

‘Yeah that’s my baby,’ ndio lilikuwa jibu la Papers katika mahojiano aliyofanya Ijumaa iliyopita kipindi cha TV Dish Nation.

lil kim-1

Rapper huyo wa New York pia alitweet picha zake na Lil Kim na kuandika ‘Yeah, that’s my baby!’.

Katika mahojiano hayo Papers aliongeza kuwa yeye na Kim wako pamoja, ‘No we are together, ‘That’s my wife. He [the baby] gonna be a Gemini.’

Lil Kim (39) ambaye atakapojifungua huyu ndiye atakuwa mtoto wake wa kwanza, amesema kuwa kwake mjamzito hakutambadilisha kwani ataendelea na shughuli zake kama kawaida na kubwa zaidi ataendelea kuwa hardcore.

‘I’m still going to work,’ aliiambia Us Weekly. ‘I’m still going to be hardcore. The baby has made me even more of a beast!’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents