BurudaniHabari

Mr Huba: EP’s zimeshusha soko la Album Tanzania

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mr. Huba amedai kuwa EP’s (Extended Play) kwa hapa Tanzania zimeanza kushusha soko la Album hapa Tanzania.

Mr. Huba amesema kuwa kwasasa wasanii wengi sio Wachanga wala wale Wakubwa wote wamekuwa wakitoa EP’s na zote zimekuwa na mafanikio sokoni.

Kuhusu soko la Album, Mr. Huba amesema kuwa soko lake kwasasa ni gumu na pia uandaaji wake ni gharama kubwa kuliko EP.

‘Kwasasa kila msanii sio mdogo wala mkubwa wote haipiti mwaka utasikia anaachia EP, Hii ni kweli soko la EP limekua kubwa kuliko Album na pia gharama za uandaaji wa Album zimekuwa juu kiasi kwamba hata kurudisha fedha za uandaaji wa Album ni ngumu”, Amesema Mr. Huba akihojiwa na Bongo5.

Akielezea sababu za Wasanii wengi kukimbilia kuachia EP’s badala ya Album, Mr. Huba amesema kuwa gharama na soko ndio chanzo kikubwa cha wasanii wengi kutoa EP.

“EP yenyewe inakuwa na nyimbo chache kuanzia 2 hadi 5, Hivyo uandaaji wake unakuwa na gharama ndogo kulinganisha na Album ambayo inatakiwa ujipinde sana kwani nyimbo zinakuwa zaidi ya 10”, amesema Mr. Huba.

Mr. Huba ambaye kwasasa anafanya vizuri wa wimbo wake wa ‘TIYARA’ amewaahidi mashabiki wake kuwa wiki ijayo anaachia kazi nyingine ambayo anaamini itakuwa kubwa zaidi ya ‘TIYARA’, Bofya link hapo chini kutazama ngoma yake hiyo ya Tiyara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents