Uncategorized

Msanii Jessica aliyeshinda tuzo ya ujasiriamali Afrika afungua shule ya mtandaoni (Video)

Binti Mtanzania Jessica ambaye pia ni msanii wa Injili kupitia kundi la J Sisters, hivi karibuni alishinda tuzo kama Mjasiriamali bora Afrika katika tuzo zilizotolewa nchini Zambia kutoka na juhudi zake katika fashion, elimu pamoja muziki, wiki hii amezungumza na Bongo5 kuhusu shule ya mtandao ambayo ameianzisha.

Jessica amesema baada ya mwaka 2019 dunia kupokea changamoto kubwa la virusi vya corona na kufanya wanafunzi wengi kukaa nyumbani bila kusoma, yeye aliamua kuanza kutafuta njia ambayo itawasaidia wanafunzi kusoma hata wakiwa nje ya shule.

Kwa sasa binti huyo ni Mkurugenzi wa shule ya mtandao Assumpter Girls Digital Nursery, Primary and Secondary Schools ambapo mpaka sasa ana wanafunzi 80 ambao wameanza masomo.

Amesema kwa kuwa mfumo huo wa elimu mtandaoni ni mgeni hivyo wanalazimika wanafunzi wengi kuanzia shule ili waanze kwanza kuuwelewa mfumo.

Pia Jessica ni muimba kwaya kupitia kundi la J Sisters.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents