Burudani

Msimu mpya kwa Watanzania umewadia tunajipanga vipi?

Nimekuwa nikisita namna ya kuanza mwaka! Kwa wale ambao hatujaonana Heri ya Mwaka Mpya. Leo ninakuja na neno muhimu. Msimu mpya umewadia na vitu vingi vinaenda kubadilika hata kama tunataka au hatutaki wakati wote unapoingia kwenye msimu mpya lazima mabadiliko yatokee yawe mazuri au mabaya ila mabadiliko yatatokea.

tanzania_640

Kwa watanzania wenzangu msimu wa nne wa kiuongozi katika nchi yetu unakwisha na kukaribisha msimu wa tano, hizo ni nyakati tano tofauti katika historia na maisha ya watanzania ingawa kuna wale ambao upofu wao ni mkubwa kiasi kwamba huwa hawaoni mabadiliko katika nyakati hizo zote.

Tutakuwa na wakati mgumu sana wa kujua mbivu na mbichi ili kuweza kuishi maisha mengine ya miaka kama kumi endapo hatutafanya mabadiliko kwa miaka mitano ya kwanza kwa msimu wa tano wa uongozi.

Kwa maisha ya kawaida ni kwamba ukishindwa kupanga umepanga kushindwa hiyo haina ubishi. Maisha ambayo tutaishi miaka ijayo yatategemea sana maamuzi ambayo tutafanya kama watanzania mwaka huu. Uchumi, elimu, afya michezo na utamaduni utategemea sana maaamuzi hayo. Je tumejipanga vipi?

Kwa wale waliosoma kitabu cha jamaa mmoja aliyeuza maisha yake ya baadaye kwa mlo mmoja na mwishowe anasema aliibiwa, ukweli wa mambo ni kwamba aliangalia tatizo lake la sasa na kuruhusu mtu ambaye akagundua fursa ya miaka mingi baadaye. Watanzania wenzangu na mimi tunahitaji kufikiri kwa makini kujipanga na kuangalia mbele zaidi ya hivyo tunavyoangalia sasa.

Mwenye kushika jembe akalime, mwenye kalamu na aandike na mwenye kucheza na acheze ni msimu mpya na majira mapya. Mambo hayatakuwa kama kawaida. Jifunze na ufahamu, chukua hatua.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents