Burudani

Mtoto wa Dully Sykes kufanya wimbo na Diamond ama Ommy Dimpoz

Msanii na mtayarishaji wa muziki, Dully Sykes ambaye pia ni baba wa watoto watatu Turiano, Misky na Moureen amesema kuwa mwanaye mmoja ameonyesha uwezo mkubwa wa kuimba ambapo tayari ameshamaliza kurekodi wimbo atakaowashirikisha Diamond ama Ommy Dimpoz.

928361_893003954062813_363585301_n
Watoto wa Dully, Turiano, Misky na Moureen

Akizungumza na Enewz ya EATV, Dully alisema mwanaye huyo amekwishamaliza kurekodi sehemu yake katika ngoma hiyo huku wakimsubiri Diamond ama Ommy Dimpoz.

“Bwana mimi watoto wangu wote naona wanafuata muziki na tayari mmoja ana nyimbo na Diamond ni kati ya hawa wawili Diamond ama Ommy Dimpoz kati ya hao watu wawili watafanya nao kwa sababu yeye ameshafanya vocal bado kati ya watu hao wawili kufanya na Nay Wa Mitego pia. Mmoja tayari ameshaonyesha kipaji cha kuimba mwingine anapenda pia kuimba na mitindo halafu mwingine ni mpole lakini anaweza akapenda pia,” alisema Dully Sykes.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents